Wakenya leo wanashiriki katika zoezi la kupiga kura ya urais katika uchaguzi mpya baada ya mahakama ya juu ya nchini humo kuubatilisha ushindi wa rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa mwezi Agosti.
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amewahimiza wafuasi wake kutoshiriki katika uchaguzi huo wa leo.
Hali ya wasiwasi imetanda huku ikihofiwa kwamba huenda kukazuka vurugu.
Wafuasi wa rais Uhuru Kenyatta, ambaye anawania awamu ya pili ya uongozi wa taifa la Kenya hapo jana walisherehekea pale walipopata habari kwamba zoezi la kupiga kura litaendelea baada ya Mahakama ya juu kushindwa kuendelea kusikiliza na kutoa maamuzi ya kusitisha kura hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta amesema hali ya usalama itaimarishwa nchini kote na amewataka Wakenya kwenda kupiga kura huku wakizingatia haki za wale ambao hawataki kushiriki katika upigaji kura.
Marekani imetoa mwito kwa Wakenya kudumisha amani na kuepukana na vurugu.
Home
Kimataifa
Slider
Upinzani nchini Kenya umewataka wafuasi wake kutoshiriki katika uchaguzi wa marudio leo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment