Wageni 98 wakamatwa mjini İzmir wakijaribu kusafiri kuelekea katika kisiwa cha Chios kinachomilikiwa na Ugiriki.
Kikosi cha kulinda pwani mjini Izmir kimefahamisha kuwa maboti mawili ya plastiki yamekamatwa yakiwa na wahamiaji 98 wakijaribu kuingia katika kisiwa hicho cha Ugiriki.
Wahamiaji hao waliokamatwa ni raia kutoka Syria, Iraq, Eritrea na Angola.
Miongoni mwa wahamiaji waliokamatwa wamo watoto na wanawake.
Baada ya kikosi hicho cha walinzi wa pwani kuwakamatwa kiliwaelekeza katika kituo cha afya mjini İzmir.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment