Image
Image

Mbeya City hawatishwi na Simba, wasema washaa soma alama za nyakati.

MBEYA City wamemaliza shughuli mapema baada ya kocha msaidizi wa timu hiyo, Mohamed Kijuso, kusoma mbinu za Simba kabla ya kukutana Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Dar es Salaam.
Kijuso alikuwa jukwaani kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kufuatilia mchezo wa ligi hiyo uliozikutanisha Yanga na Simba, uliochezwa Jumamosi iliyopita na kumalizika kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Akizungumza na BINGWA jana, Kijuso alisema amefanikiwa kusoma udhaifu wa Simba na benchi la ufundi la Mbeya City, wanafanyia kazi ili waweze kushinda mchezo huo.
Kijuso alisema wanaendelea kujipanga na Simba wasitarajie ushindi rahisi kwao, kwani malengo yao ni kubakisha pointi tatu nyumbani.
“Simba ni timu kubwa ambayo niliwahi kupita, ila msimu huu wanaonekana kujipanga sana hasa usajili wao lakini sisi kama Mbeya City hatuna hofu yoyote, tunawasubiri na kama walitarajia mchezo utakuwa mteremko kwao tunawaambia wasijidanganye,” alisema.
Alisema katika mchezo huo dhidi ya Simba, wanatarajia kumkosa mchezaji wao, Frank Hamis, ambaye ana kadi tatu za njano lakini pengo lake litazibwa na wengine.
Katika mchezo wao uliopita uliochezwa Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Azam FC, kikosi hicho cha Mbeya City, kilikubali kichapo cha bao 1-0 na sasa wanataka kumalizia hasira kwa Simba.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment