Wizara ya fedha na mipango imekanusha taarifa zinazosambaa kuwa deni la taifa limepitiliza ukomo wa kiasi kilichopangwa kimataifa na kusisitiza kuwa deni la taifa kwa pato la taifa ni stahimilivu kwani mpaka sasa Tanzania imefikia asilimia 32 huku ukomo ikiwa ni asilimia 50.
Katibu mkuu wa wizara ya fedha na mipango Doto James ametoa kauli hiyo wakati wa kusaini makubaliano ya kupokea mkopo wa shilingi bilioni 340 kutoka benki ya dunia kwa ajili ya mradi wa kuboresha miundombini ya vivutio vya sekta ya maliasili na utalii nyanda za juu kusini mkoani iringa mradi unaotarajiwa kuibua fursa zaidi kiuchumi.
Kwa upande wake katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii meja Generali Gaudence Milanzi ameshukuru benki ya dunia katika kufanikisha mradi huo ambao utachangia kuboresha miundombinu ndani na nje ya hifadhi hivyo kuzitangaza fursa ya shughuli za kitalii nchini.
Kuboreshwa kwa miundombinu katika vivutio hivi katika hifadhi na maeneo yanayozunguka eneo la Iringa kutachangia kuikuza sektra ya utalii ambayo inachangia asilimia 17.2 katikapato la taifa kwa kuchangia asilimia 25 ya fedha za kigeni nchini.
Home
News
Slider
Taarifa zinazodai deni la taifa limepitiliza ukomo wa kiasi kilichopangwa Kimataifa zakanushwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment