Image
Image

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete yafanya upasuaji mkubwa mshipa unaotoa damu kwenye moyo .

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa mara ya kwanza hapa nchini imefanya upasuaji wa kurekebisha mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zingine za mwili katika kambi maalum ya upasuaji ya siku sita katika mkutano na waandishi wa habari hospitalini hapo jijini Dar es salaam.
Daktari wa moyo kutoka katika taasisi hiyo Dkt. Bashir Nyangasa amesema katika kambi hiyo ya siku sita kwa kushirikiana na hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India wamefanikiwa kuwafanyia upasuaji mkubwa wa moyo wagonjwa 15 ambao wote afya zao zinaimarika Dkt. Nyangasa amesema upasuaji huo umesaidia serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kwani endapo wagonjwa hao wangekwenda kutibiwa nje ya nchi ingetumia zaidi ya milioni 405,gharama ya mgonjwa mmoja ikiwa Milioni 25 ukilinganisha na gharama waliyotumia katika taasisi hiyo sh Milioni 225 tu kwa wagonjwa wote 15.
Taasisi hiyo imeendelea kusisitiza wananchi kufika katika hispitali hiyo kujitolea kuchangia damu kutokana na kuhitajika kwa wingi kwani mgonjwa anayefanyiwa upasuaji huhitaji damu kati ya chupa 5 hadi 6.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment