Image
Image

Wanachama 50 wa CHADEMA wahamia CCM, wasema wanaridhishwa na kasi ya Magufuli.

Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo baada ya kuondokewa na wanachama 50 mkoani Geita ambao wamehamia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Vijana  hamsini wanachama wa CHADEMA kutoka kijiji cha Buligi kata ya Senga wilayani Geita wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Katibu wa UVCCM wilayani Geita Bw. Ali Rajab alisema vijana hao wamehama Chadema na kujiunga na CCM kutokana na kasi ya utendaji ya Rais Magufuli.
Katika kampeni hizo  Bw. Rajab amewataka watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na Chama cha Mapinduzi CCM kwa ujumla kwani bila kufanya hivyo.
Naye Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake, UWT wilayani Geita Bi. Mazoea Salim, amesema CCM inatarajia kushinda kwenye uchaguzi huo mdogo katika kata ya Senga kutokana na uwezo wa mgombea ambaye wamemsimamisha.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment