Waziri wa afya na Ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi amesema baadhi ya wagonjwa wa kisukari nchini wamepoteza viungo mbali mbali ikiwemo kukatwa miguu, kupoteza macho na matatizo ya figo, kunatokana na kuchelewa kufika katika vituo vya kutolea Huduma ya afya.
|
Dk. Hussein Mwinyi - Waziri wa afya na ustawi wa Jamii |
Dk. Mwinyi ameyazungumza hayo wakati wa uzinduzi wa Kliniki inayotembea maalumu kwa wagonjwa wa kisukari inayotembelea wagonjwa wa kisukari itakayo jikita zaidi maeneo ya vijijini, yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 40, uliofanywa kwa ushirikiano baina wizara ya hiyo na chama cha wagonjwa wa kisukari Tanzania TDA.
Hata hivyo amewataka wananchi katika maeneo husika kuunga mkono jitihada za chama cha wagonjwa wa kisukari na kutumia fursa hiyo kuchukua hatua mapema kwenda kupima afya zao, ili kuepuka matatizo kama hayo ya kupoteza viungo, jambo ambalo linachangia pamoja na mambo mengine kuongezeka kwa umasikini nchini
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment