Image
Image

EXCLUSIVE: MKUU WA JESHI LA POLISI IGP SAIDI MWEMA ATUMA KIKOSI KAZI WILAYANI LIWALE KUFUATIA VURUGU ZILIZOIBUKA , 19 WANASHIKILIWA KWA MAHOJIANO.

IGP Said Mwema - Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema ametuma timu maalum ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCP Issaya Mngulu kwenda kuongeza nguvu wilayani Liwale mkoani Lindi kufuatia vurugu zilizotokea Wilayani  humo jana jioni.

Advera  Senso - Msemaji Jeshi la Polisi
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la polisi ADVERA SENSO  imeeleza kwamba mpaka sasa jumla ya watuhumiwa kumi na tisa  wamekamatwa kwa mahojiano baada ya kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni wakulima wa Korosho kujaribu kuzuia gari lililokuwa na malipo ya korosho wakipinga malipo ya pili ya Korosho ambapo walianza kufanya vurugu na uharibifu mkubwa wa mali.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa nyumba kumi na nne zimechomwa moto, baadhi ya mifugo imejeruhiwa na kuangamizwa na kufanyika uharibifu wa miundombinu ya barabara.

Jeshi la Polisi nchini limelaani vitendo hivyo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi na badala yake kuwataka kufuata njia ya kufanya majadiliano pale ambapo kutakuwa na migogoro ya aina yoyote ndani ya jamii.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment