Image
Image

SERIKALI YAZUNGUMZIA KUSUDIO LAKE LA KUANZA KUTEKELEZA MPANGO MAALUM KATIKA SEKTA YA MAJI ILI KUKABILIANA NA TATIZO KUBWA LA MAJI NCHINI.

Serikali inakusudia kuanza kutekeleza mpango maalum katika sekta ya maji utakaoleta matokeo ya haraka kuanzia mwaka ujao wa fedha, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na tatizo kubwa la maji nchini.

Hayo yameelezwa bungeni mjini Dodoma na waziri wa maji, Profesa Jumanne Maghembe, wakati alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2013/2014, na kusisitiza kuwa mpango huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu.
Profesa  Jumanne  Maghembe Waziri wa Maji
Profesa Maghembe amefafanua kuwa mpango huo utatekelezwa katika kuongeza idadi ya vituo vya kuchotea maji, kuboresha usimamizi wa miradi ya maji na kuboresha mfumo wa upatikanaji wa vipuli vya mitambo ya maji.

Hata hivyo, pamoja na serikali kutoa matumaini hayo mapya, Kamati ya bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake na Mbunge wa Sikonge, Bw. Saidi Nkumba, imeonyesha kutoridhishwa na kiasi kidogo cha fedha kilichotengwa katika wizara hiyo, wakati mahitaji ya maji yakiwa yanaongezeka.

Kwa mujibu wa jedwali la kamati hiyo, fedha za matumizi ya kawaida katika wizara hiyo zimekuwa zikipungua kutoka shilingi bilioni 16.8 mwaka 2006/2007 hadi kufikia shilingi bilioni 3.8 mwaka 2012/2013.
Kwa upande wake, Kambi ya Upinzani bungeni kupitia kwa msemaji wake, mbunge wa viti maalum (CHADEMA) Bi. Cecilia Pareso,  imeitaka serikali kudhibiti vitendo vya kifisadi katika sekta hiyo, na ikatolea mfano wa mradi wa kukarabati na kupanua miundombinu ya maji safi na maji taka katika jiji la Dar es Salaam, maarufu kama mabomba ya wachina, ambapo kiasi cha dola za kimarekani milioni 164.6 kilitumika, lakini mabomba hayo hayatoi maji.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment