Na. Kuringe Mongi, Dodoma
Pamoja na serikali kukubali kuongeza shilingi bilioni 184.5 katika miradi ya maji, spika wa bunge leo imembidi kusitisha kikao cha bunge kabla ya wakati, ili kutoa nafasi kwa serikali kujiandaa kutoa ufafanuzi ni mafungu gani yaliyomegwa ili kupata kiasi hicho cha fedha.
|
Bi. Anne Makinda - Spika wa Bunge Tanzania |
Spika wa bunge Bi. Anne Makinda ilimbidi kuchukua uamuzi huo baada ya kuombwa miongozo mitatu mfululizo kutoka kwa wabunge wa Kambi ya Upinzani.
|
Kabwe Zitto. Kigoma Kaskazini |
|
Tundu Lissu - Singida Mashariki |
|
John Mnyika - Ubungo
Akitoa muongozo wake, Spika Makinda amesema kwa maana ya wizara ya maji ni lazima waletewe marekebisho ya vifungu vya fedha, ili waweze kupitisha kwa usahihi, lakini akatolea ufafanuzi kuhusu kuruhusiwa waziri wa fedha Profesa William Mgimwa kutoa kauli bila ya kuwepo kwa nakala, kama kanuni za bunge zinavyotaka.
|
Naye, Mtoa hoja, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe akijibu hoja za wabunge, amesema kuanzia sasa wizara yake imefuta vibali vyote vya utekelezaji wa miradi ya maji, na miradi hiyo itasimamiwa na halmashauri husika.
|
Prof. Jumanne Maghembe - Waziri wa Maji |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment