Image
Image

EXCLUSIVE: SIMANZI, HUZUNI ZA TAWALA DSJ, WAPOTEZA MPENDWA WAO MWANAHABARI CHIPUKIZI.


Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari( DSJ) wapo katika simanzi kufuatia Msiba wa Mwanafunzi mwenzao ambaye ni waziri chuoni hapo kufariki dunia kwa ajali ya gariBaada ya gari yao  Kugongana uso kwa uso na lori la Mafuta katika  Maeneo ya Chalinze Jijini Dar es Salaam wakati wakirudi, sambamba na dereva wa gari hilo  wakati wakitokea mkoani mbeya kwa ziara ya Kimasomo.

Mapema leo kiongozi wa Msafara chuoni hapo Bwana VICTOR SINKA  amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu wawili, Akiwemo DIEDON KIBONA ELIANSON ambaye alikuwa mwanafunzi chuoni hapo, Pamoja na ALLY ZUNGU ambaye ndie alikuwa dreva wa gari hilo, huku akieleza kuwa wanafunzi wengine wawili wamelazwa katika Hospitali ya Tumbi kibaha kwaajili ya matibabu  Huku hali zao zikiwa sinzuri, na wengine 18 wakiwa wameruhusiwa licha yakuwa wanamaumivu sehemu mbali mbali za miili yao.
 MAREHEMU DIEDON KIBONA ELIANSON - ENZI ZA UHAI WAKE
Amesema ingawa wakati wakiwa wanarudi kutoka mbeya kuja  Dar es Salaamu njiani  walikutana na misuko suko mbali mbali bara barani, licha yakuwa kunagari yao iliweza kupata pancha barabarani, lakini waliweza kuondoka morogoro vizuri 2 ila mara baada ya kufika chalinze na kama ilivyokuwa kwamba ni usiku waliliona lori la mafuta likiwa mbele yao huku likiwa linayumba, jambo ambalo lilimfanya Dreva aliyekuwa akiendesha gari hilo lililokuwa limebeba wanafunzi hao kujaribu kulikwepa lakini ilishindikana na hatimaye kukutana uso kwa uso na lori hilo na kusababisha ajali hiyo.

Kwenye loro hilo kulikuwa na mwanamke na mwanaume ambapo mara baada ya kutokea ajali hiyo Bwana Sinka alisema hawakuweza kumuona mwanamke aliyekwa ndani ya lori hilo, huku dreva wa ori hilo naye ikielezwa hali yake haikuwa ya kuridhisha.

Alisema baada ya ajali majeruhi walipelekwa kwenye Dispensary ya chalinze jambo ambalo ililazimu kupelekwa tumbi kwaajili ya matibabu, kutokana na dispensary hiyo kukosa dawa na hivyo kuwaladhimu kujinunulia dawa wenyewe ili kuweza kuwapatia majeruhi huduma ya kwanza.

Pia wakati kuwaokoa ndugu na jamaa kwa lengo la kunusuru maisha hali ilikuwa siyakuridhisha kutokana na watu waliokuwa wakiwasaidia kuokoa, kuanza kuwaibia vitu mbali mbali walivyokuwa navyo ikiwemo kamera jambo ambalo uongozi wa chuo hicho umesikitishwa nacho, na mmoja wa wanafunzi kutishiwa maisha katika eneo hilo la ajali kwa kile kilicho elezwa kuwa alikuwa anadai mizigo na thamani zinginezo ambazo zilikuwa ni mali zao na hatimaye kuambiwa kuwa" Kuwa saidia kuokoa tumewasaidia sasa na mizigo hii una taka hii ni yakwetu, ondoka tusije tukakumaliza" alisema sinka katika nukuu.

Hata hivyo miili ya marehemu hao ipo katika hospitali ya tumbi, ambapo kwa upande wa marehemu DIEDON KIBONA yeye mazishi yanatarajiwa kufanyika mbezi jijini Dar es Salaam, lakini marehemu nyumbani kwao ni mtu wa Tabora.

Uongozi wa Dsj umesema utashirikiana na ndugu na jamaa wa mfiwa huyo katika kipindi hiki kigumu lakini kwa chuo hicho kumeachwa pengo ambalo alitoweza kuzibika.

Aidha katika msafara wao ya  ziara ya kimasomo kulikuwa na magari 6,walimu watatu akiwemo kiongozi wa msafara huo. 

Kwa taarifa zaidi juu ya shughuli za mazishizinavyo endelea tutawajuza licha ya kwamba blog hii inaendelea kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa pwani kuthibitisha hili, 

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU DIEDON KIBONA MAHALA PEMA AMEN. 

   


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment