Na Kuringe Mungi, Dodoma.
Jamii nchini imehimizwa kuwa na wajibu wa kulea watoto yatima na siyo kuliacha jukumu hilo kwa serikali na hivyo kusababisha kuwepo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Wito huo umetolewa mjini Dodoma na Mke wa Waziri Mkuu Bibi. Tunu Pinda, wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla fupi ya Catherine Development Foundation, kukabidhi zawadi kwa watoto yatima wa kijiji cha Matumaini.
|
Tunu Pinda - Mke wa Waziri Mkuu
Hata hivyo naye , Mkurugenzi wa mfuko huo wa maendeleo ambaye pia ni mbunge wa viti maalum (CCM) Bi. Catherine Magige, alichukua wasaa huo kuwahasa watoto hao kujibidiisha kwenye masomo, ili waweze kuzifikia ndoto njema katika maisha yao ya huko mbeleni.
|
|
Catherini Magige - Mbunge Viti Maalum CCM |
Katika hafla hiyo, Mfuko huo wa Maendeleo wa Catherine ulitoa zawadi mbalimbali za vyakula na nguo kwa kituo hicho cha malezi ya watoto yatima, hatua ambayo iliungwa mkono na mke wa Waziri Mkuu kwa kutoa pia zawadi mbalimbali.
Jumuiya hiyo ya Kijiji cha Matumaini kilitoa shukrani zake za dhati kwa wageni wao kwa kuonyesha moyo wa upendo na kuwathamini watoto hao yatima.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment