Kocha wa Timu ya Soka ya Taifa "Taifa Stars", Kim Poulsen ametangaza timu ya pili ya Taifa (Young Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji ambao baadaye anaweza kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kabla ya kutaja kikosi hicho, Kim amesema timu hiyo ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza vipaji vya wachezaji.
|
Kim Poulsen - Kocha Mkuu - Taifa Stars
Amesema timu hiyo inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa Stars, na kwa hiyo atatumia Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.
|
Naye Kocha wa Timu za Taifa za Vijana Jakob Michelsen naye amesisitiza umuhimu wa timu hiyo yenye wachezaji 30 ambayo itakuwa na kambi ya siku tano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu, ambapo Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la soka nchini TFF Sunday Kayuni amesifu mpango huo.
|
Jakob Michelsen - Kocha Timu za Taifa za Vijana |
Aidha baadhi ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni kipa Ali Mustapha "Barthez" wa Yanga, David Mwantika wa Azam, Vicent Barnabas wa Mtibwa Sugar, Ramadhani Singano na Miraji Adam wa Simba.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment