Rais Uhuru Kenyatta ametangaza baraza jipya la mawaziri lenye watu kumi na wanane, baraza ambalo limekuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na raia wa nchi hiyo Tangu alipoapishwa kushika kushika uongozi ikiwa ni awamu ya nne.
|
Uhuru Kenyatta - Rais wa Kenya |
Rais Kenyatta na Naibu wake William Rutto wamekuwa wakiwaahidi wananchi wa kenya kuwa wataunda safu yenye viongozi wachache, lakini iliyobora kwa lengo la kuweza kuhimili majukumu ya kuiendeleza Kenya na watu wake.
Kufuatia ahadi hiyo, Hivi karibuni Rais Kenyatta alitoa muundo wa wa serikali yake aliyotarajia kuiunda , ambapo alipunguza wizara kutoka 44 zilizokuwepo katika utawala wa mtangulizi wake Rais Kibaki na kubakiza wizara 18.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment