Ligi ya Mabingwa wa Mikoa ya kutafuta timu tatu zitakazopanda kucheza
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao chini ya usimamizi wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itaanza Mei 12 mwaka huu.
Uwasilishaji wa jina la bingwa wa mkoa unatakiwa kufanyika pamoja na
ulipaji ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000. Mfumo wa ligi hiyo ni
bingwa wa mkoa X kucheza na bingwa wa mkoa Y nyumbani na ugenini ambapo
mshindi ndiye anayesonga mbele katika hatua inayofuata
Mwisho wa mikoa kuwasilisha majina ya mabingwa wao ni Mei 1 mwaka huu
wakati ratiba ya ligi hiyo itapangwa mbele ya waandishi wa habari Mei 3
mwaka huu kwenye ofisi za TFF.
Usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika hatua
ya mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF
inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya
ligi hiy
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment