Image
Image

RIMOTI KONTRO KUWAONGOZA MAKINDANDA NA NAIBU WAKE.

SPIKA wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Anne Makinda ameungana na Naibu wake Job Ndugai na kugonga msunari wa mwisho katika kifungo cha siku tano dhidi ya wabunge wa Chadema waliosimamishwa kushiriki vikao vya bunge kwa siku tano.
 
Spika Makinda aligonga msumari huo baada ya Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe kuomba mwongozo kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano kwa wabunge watano wa Chama hicho.
Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Anne Makinda
Hata hivyo Spika Makinda alidai kwamba uamuzi wa Naibu Spika ulkuwa sahihi na kwamba hakuna kanuni kuhusu jambo hilo na kwamba uamuzi huo utabaki kama ulivyo kwa kuwa ni halali na zaidi utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi endapo jambo hilo litatokea tena wakati wa vikao vya bunge.
 
Hata hivyo wakati Makinda akiungana na Naibu wake, wasomi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini wamepinga vikali uamuzi huo na kudai kwamba bunge la sasa linaongozwa kwa rimoti kontro.

Wakizungumza katika kipindi maalum kilichorushwa hewani jana kwenye kutuo cha luninga cha ITV wasomi hao walidai kwamba Spika ameshindwa kuliongoza bunge ipasavyo badala yake kuna watu wanaoliongoza bunge hilo rimoti wakiwa nje.

Wabunge hao ni Lissu, Hezekiah Wenje (Nyamagana), Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) Godbless Lema (Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini). Chanzo za kufukuzwa kwao ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment