Hatua
hiyo imekuja kufuatia mchango wake katika kuitangaza sanaa ya Zanzibar
nje ya mipaka ya Tanzania hasa kwenye fani ya muziki wa Taarabu asilia
na ile ngoma maarufu ya Unyago inayotumika katika sherehe za harusi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo
wakati akiifariji familia ya Marehemu Bi. Kidude wakati wa matayarisho
ya mazishi yake eneo la Rahaleo nyuma ya Kituo cha ZBC Redio Rahaleo
Mjini Zanzibar.
Balozi
Seif akitoa ubani wa shilingi Milioni (2,000,000/- )kwa niaba ya Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa familia ya marehemu amesema jamii na
waswahili wote katika mwambao wa Afrika Mashariki wanafahamu mchango
mkubwa wa Msanii Bi. Kidude katika fani ya muziki wa taarabu.
Amesema
Zanzibar imepata sifa kubwa katika Nyanja za Kimataifa kutokana na
mchango wa wasanii kwa kueneza sanaa ya Taarabu iliyotoa fursa kwa
baadhi ya watalii na wataalamu kuvitembelea Visiwa vya Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameitaka Familia ya Msanii Bi. Kidude kuwa
na moyo wa subra katika kipindi hichi kigumu cha msiba na kuwaeleza
kwamba msiba huo sio wao peke yao.
Balozi
Seif amesema kwa kweli sisi sote tulimpenda sana Bi. Fatma Binti Baraka
(Kidude) lakini tuelewe kwamba Mwenyezi Mungu amempenda zaidi na ndio
maana akamuhitaji.
Naye
Mmoja wa wana Familia hiyo Bw. Haji Ramadhan Suwed Buda kwa niaba ya
Familia ya Marehemu Bi. Kidude ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa mchango wake wa kuungana nao katika msiba huo.
Bw. Haji amesema hatua hiyo ya Serikali imeleta faraja kwao na kupunguza machungu ya msiba huo.
Msanii
Gwiji wa sanaa ya Taarab asilia na ngoma ya Unyago Marehemu Bi. Kidude
aliyekadiriwa kufikia umri wa zaidi ya miaka 98 hakuwahi kuolewa wala
kupata Mtoto.
KWANIABA YA MASINDA.
0 comments:
Post a Comment