Matumizi ya mashine za risiti za kielektronik kwa wafanyabiashara waliosajiliwa na kodi la ongezeko la thamani -VAT yamechangia kuongezeka kwa mapato ya kodi tangu mfumo huo ulipoanza kutumika Julai mwaka 2010 ikiwa ni awamu ya kwanza.
Generose Bateyunga - Naibu Kamishna - Idara ya Kodi za Ndani - TRA |
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina ya kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya mashine hizo kwa wafanyabiashara wa kipato cha kati jijini Dar es salaam, naibu kamishna Idara ya kodi za ndani ya Mamlaka ya Mapato Nchini -TRA Generose Bateyunga amesema kwa mwaka wa fedha 2010/2011 mapato ya kodi kwa wafanyabiashara waliosajiliwa na VAT yaliongezeka kwa asilimia 9.6 huku mwaka 2011/2011 ongezeko hilo likifikia asilimia 23.
Bi Bateyunga amesema mapato ya kodi yataongezeka zaidi katika mwaka wa fedha ujao hasa baada awamu ya pili ya mfumo wa matumizi ya mashine za risiti za kieletronic kwa wafanyabiashara wa kati wasiosajiliwa na VAT itakapoanza Mei 15 mwaka huu.
Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki semina hiyo wameelezea faida katika matumizi ya mashine hizo huku baadhi wakielezea changamoto zilizopo katika utumiaji wa mashine hizo kama vile kuharibika.
Mashine za risiti za elektronik ni mfumo ulioanzishwa na TRA ili kurahisisha ukusanyaji na ulipaji wa kodi na kumwezesha mfanyabiashara kutunza kumbukumbu zake ambazo zitasaidia kuondoa malalamiko wakati wa ulipaji wa kodi, pamoja na ulipaji kodi kufanyika kwa uwazi na uaminifu.
-------------------------------------------------------------------------
0 comments:
Post a Comment