Image
Image

EXCLUSIVE: TANZANIA MBIONI KUTIMIZA MALENGO YA MILENIA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

Tanzania ni miongoni mwa nchi sita barani Afrika zinazoelekea kutimiza malengo ya milenia  katika  kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto walio na umri chini ya miaka  mitano.

Akizungumza wakati wa hafla ya kutimiza miaka 40 ya shirika la kimataifa la 'jh piego ' jai piego la marekani linalojishughulisha na utoaji huduma za afya kwa mama na mtoto, mafunzo kwa wakunga na wauguzi hapa nchini ,Naibu waziri wa Afya Dr.Seif Rashid amesema vifo  vya watoto chini ya umri wa miaka mitano vimepungua kutoka 147 kwa mwaka 1999 na kufikia vifo 65 mwaka 2012.
.Dr.Seif  Rashid -Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.
Amesema katika vizazi 1000 vya watoto kila mwaka vifo vimepungua hadi kufikia 45 kwa mwaka huku vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi vikiwa vimepungua kwa asilimia kubwa kwa mujibu taarifa iliyotolewa mwaka 2012 ya shirika la afya duniani.
Mama Mjamzito
Aidha Naibu waziri huyo wa afya amesema katika kupambana na maambikizo ya ugonjwa wa ukimwi, shirika hilo limefanikiwa kuwafikia wanaume 1500 kwa kuwafanyia tohara katika mkoa wa Iringa pekee mwaka jana.

Nae Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema serikali itaendelea kushirikiana na mashirika ya kimataifa katika kuleta ustawi wa jamii hasa katika kupambana na vifo vya mama mjamzito na mtoto huku rais wa shirika la JH PIEGO pamoja na mwakilishi wa shirika la kimataifa la misaada la marekani wakiahidi kuendelea kuisaidia Tanzania hususan katika nyanja za kiafya ili kufikia malengo ya milenia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment