Jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni linamshikilia mtu aliyefahamika kwa jina la Tito Omeme mkazi wa mwenge jijini dsm kwa tuhuma za kumshambulia na kumnyonga mikono askari wa usalama barabarani mwenye namba F.6003 Idiphone kwa nia ya kunyang'anya funguo ya gari la mtu huyo wakati akitekeleza majukumu yake.
|
ACP Charles Kenyela - Kamanda wa mkoa wa kinondoni |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam, Kamanda wa mkoa wa kipolisi kinondoni ACP Charles Kenyela amesema jeshi hilo linaalaani kitendo cha kudhalilishwa askari polisi akiwa kazini na kuwataka wananchi kujenga utamaduni wa kuheshimu na kuzingatia sheria mbalimbali ikiwemo kuepuka kutumia nguvu pindi wanapotakiwa kujisalimisha katika mikono ya polisi.
Amesema chanzo cha vurugu hizo inadaiwa kulitokana na Tito ambaye alikuwa na gari ndogo aina ya toyota chaser kumchomekea dereva wa daladala na kufunga barabara ya mwenge hivyo kusababisha msongamano ambapo askari huyo aliingilia kati na kujikuta akishambuliwa na mtuhumiwa huyo mbele ya umati wa watu.
si Kinondoni.
Jeshi hilo limewaonya wananchi hasa wanaotumia barabara kuzingatia sheria ili kuepuka migongano isiyokuwa ya lazima.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment