Watoto ni njia mojawapo ya kufikisha kwa jamii elimu ya namna ya kupambana na magonjwa mbalimbali ukiwemo ugonjwa wa malaria kutokana na uwezo wao wa kujifunza, kuelewa haraka na kutosahau waliyojifunza kinyume na mtu mzima.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa malaria inayolenga shule sita za jijini Dar es salaam ambapo leo kampeni hiyo imeendeshwa katika shule ya msingi makumbusho manispaa ya kinondoni.
Malaria haikubaliki tujilinde kwa kushusha Net |
Katika utekelezaji wa kampeni hiyo, kampuni ya Total imejiunga na mpango huo mwaka jana hususani kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya malaria duniani April 25 ambapo imeendelea na zoezi la kutoa elimu kwa wanafunzi katika shule sita za jijini Dar es salaam zilizo katika maeneo hatarishi
0 comments:
Post a Comment