Lema alikwenda katika chuo hicho baada ya kuwepo kwa taarifa ya mwananzi aliyeuawa kwa kuchomwa kisu hadi kufa, ndipo jeshi hilo lilokuwa katika eneo hilo pamoja na Mkuu wa Mkoa huo Magesa Mulongo kumtuhumu na kuvuta gari lake kutokana na tukio hilo.
Kutoka na vurugu zilizokuwepo katika chuo hicho Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo aliamua kukifunga kwa muda usiojulikana huku akiwatakaka wanfunzi kuondoka chuoni hapo haraka iwezekanavyo.
Mbunge huyo alifika Chuoni hapo baada ya wanafunzi hao kuandamana mpaka nyumbani kwake iliyopo maeneo ya jirani na Chuo hicho na kufanikiwa kutuliza vurugu na jazba za wanafunzi ingawa bado alionekana kuwa chanzo cha vurugu hizo.
Lema aliamua kujificha ili kukwepa kukamatwa mbele ya wanafunzi hao, kwani ingeamsha jazba ya wanafunzi kiasi ambacho ingeongeza ruvugu zaidi kuona mbunge huyo aliyefanikiwa kutuliza vurugu zao akikamatwa tena.
Pamoja na wanafunzi hao kumficha Mbunge huyo, asikamatwe na Askari hao wa Jeshi la Polisi, bado walishindwa kuvumilia baada hatua ya jeshi hilo kuvuta gari la Lema.
Uvumilivu wa wanafunzi hao ulikwisha na kuanza kumpopoa Mkuu huyo wa Mkoa kwa mawe huku wakimtuhumu kuwa chanzo cha vurugu za Chuo hicho kutoka na kauli zake zilizojaa uhasama wa kisiasa.
Taarifa za kifo cha mwanfuzi huyo zilipokelewa kwa huzuni mkubwa chuo hapo huku kila mwanafunzi akishindwa kuzungumzia chanzo cha kifo chake kwa madai kwamba Jeshi la Polisi limeanza
0 comments:
Post a Comment