Wananchi wanaofuga wanyama wa majumbani wametakiwa kuitikia wito wa serikali kuhusu suala zima la kuwapatia chanjo wanyama wanaowafuga ili kutokomeza baadhi ya magonjwa yanayowaandama wanyama wa kufugwa.
Akisoma tamko la waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi,DK MATHAYO DAVID MATHAYO, Msemaji mkuu wa wizara hiyo.Dk. MOHAMED BAHARI, amewahimiza wananchi kuchukua nafasi ya maadhimisho ya siku ya chanjo duniani ambayo imeadhimishwa duniani kote , kuwatumia wataalam wa sekta ya mifugo na uvuvi katika kutambua magonjwa na kuhakiki ubora wa mazao husika.
|
Mnyama akipatiwa Chanjo |
Amesema tabia iliyojengeka ya kusubiri mpaka wanyama wapate magonjwa au kutumia dawa bila ya ushauri,ni kitendo kinachoweza kumletea mfugaji gharama kubwa na hasara na pia kunaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa.
|
Madaktari Wakitoa Chanjo Kwa Mbwa |
Katika hatua nyingine Dr. HENRY MAGWISHWA , Katibu wa chama cha matabibu
ya wanyama nchini TVA, amesema hadi sasa hakuna chanjo ya mnyama
nguruwe ambae pia......
|
Nguruwe |
anafugwa na kusisitiza kuwa dawa pekee inayotumika
unapozuka ugonjwa wa nguruwe ujulikanao kama shwine fever,serikali
huwasiliana na wafugaji ili kuwaelekeza namna ya kutokomeza ugonjwa huo.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment