Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi mbalimbali za elimu ya juu, wamekiri kuwa kutojiamini pamoja na matumizi ya lugha ya kiingereza kumekuwa kukichangia kwa kiasi kikubwa wengi wao kushindwa kuhimili ushindani kwenye soko la ajira, pindi fursa zinapojitokeza.
Wanafunzi hao wametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na vyombo vya habari, kwenye tamasha la makampuni mbalimbali ya kibiashara na huduma zaidi ya 20 yalipokutana na wanafunzi hao kwa ajili ya kuwajengea uwezo chini ya Mpango ulioandaliwa na Taasisi ya kuendeleza Masuala ya Uongozi kwa Vijana AIESEC.
.Frank Mushi - Rais wa AIESEC |
Wanafunzi wa Vyuo Mbali mbali wakisikiliza |
Nao baadhi ya wanafunzi walioshiriki tamasha hilo wanaeleza changamoto hizo na juhudi wanazoona zinafaa kutiliwa mkazo tangu mwanafunzi akiwa chuoni akijiandaa kuingia kwenye soko la ajira, ambapo Mwakilishi wa Vodacom Tanzania moja ya Makampuni yaliyodhamini tamasha hilo akizungumzia nafasi ya ajira kwenye makampuni.
0 comments:
Post a Comment