Image
Image

EXCLUSIVE: SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WANANCHI KUWA IMEJIANDAA KUPELEKA CHAKULA CHA MSAADA KWA FAMILIA ZILIZOKUMBWA NA UHABA WA CHAKULA KATIKA MAENEO KADHAA NCHINI.

Na .Mcharo Mrutu 

Serikali imewahakikishia wananchi kuwa imejiandaa kupeleka chakula cha msaada kwa familia zilizokumbwa na uhaba wa chakula katika maeneo kadhaa nchini na kwamba hakuna mwananchi atakayepoteza maisha kwa kukosa chakula.

Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dk Mathayo David Mathayo amesema hayo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mradi wa uboreshaji wa maisha kupitia sekta ya kilimo -LEAD unaoetekelezwa na shirika lisilo la kiserikali ya Brac Maendeleo Tanzania lililo chini ya shirika la maendeleo ya Uingereza.

Dk. David  Mathayo David - Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
 Dk Mathayo aliyekuwa akitolea ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya taarifa za baadhi ya maeneo ya nchi kukumbwa na uhaba wa chakula kutokana na kukosa mvua za kutosha, amesema tayari maafisa wa serikali wapo katika maeneo hayo kufanya tathmini na kuangalia namna ya kuzisaidia familia zilizoathirika.

Akizungumzia umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na shirika la Brac Maendeleo Tanzania ambalo kimsingi linajishughulisha zaidi kuwawezesha wakulima na wafugaji wadogowadogo kwa kuwapatia mafunzo ya namna ya kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji kwa tija, waziri Dk Mathayo amelishauri shirika hilo kushirikiana kwa karibu na maafisa ugani katika ngazi za wilaya.

Mradi huo wa miaka minne wenye thamani ya takribani shilingi bilioni 20 utatekelezwa katika mikoa 18 kwa lengo la kuongeza kipato cha wananchi wa vijijini, kuwapatia ujuzi wakulima wa mahindi na wafugaji wadogo wa kuku na kuongeza uzalishaji wa chakula, ambapo zaidi ya watu laki moja wanatarajiwa kunufaika moja kwa moja na mradi huo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment