Tukio hilo lilitokea usiku wa Aprili 20 mwaka huu, ambapo askari hao zaidi ya watano waliingia katika ukumbi wa disko wa High Way uliopo njia panda ya Himo na hivyo kutoa mwanya kwa magari sita aina ya Fuso yaliyokuwa yamesheheni sukari ya magendo kupita kirahisi kwenda nchini Kenya.
Uchunguzi
umebaini kuwa baada ya askari hao kutinga katika ukumbi huo, ilichukua muda wa
dakika 20 magari yakaanza kupita eneo hilo ambako askari hao walikuwa wameweka
doria katika barabara ya Mwika.
Mbali
na askari hao, pia maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) nao huweka doria
katika barabara hiyo ya Mwika, lakini siku hiyo waliungana na askari wale
katika ukumbi wa disko na kuacha magari hayo yakienda Kenya bila kukaguliwa.
Hata
hivyo, raia wema waliwasiliana na waandishi wa habari za uchunguzi ambapo
magari mawili yalijikuta mikononi mwa wananchi huku moja likiwaponyoka baada ya
dereva wake kukimbia na kwenda kulificha katika mji mdogo wa Himo.
Gari
lililobaki mikononi mwa wananchi wakiwamo pia waandishi wa habari za
uchunguzi lilikuwa na namba za usajili T 695 BXH aina ya Fuso mali ya Susan
Bahati Paul wa Moshi Mjini ambalo lilibainika kusheheni sukari kutoka nchini
Thailand.
Gari
hilo ambalo lilikuwa mita chache kuingia nchini Kenya kupitia eneo la machimbo
ya mchanga aina ya pozolana, lilikabidhiwa kwa maofisa wa TRA katika kituo cha forodha
cha Holili likiwa na mifuko 250 ya sukari yenye ujazo wa kilo 50 kia moja.
Alipoulizwa
jana juu ya askari wake kwenda kustarehe disko na kuacha sukari ikienda Kenya,
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita pamoja na kudai hana
taarifa, aliahidi kulishughulikia suala hilo.
Wakati
Moita akidai hana taarifa, habari za ndani ya Jeshi la Polisi zimedokeza kuwa
askari wote waliokuwa zamu mpakani hapo usiku wa kuamkia Aprili 20 mwaka huu,
wamehojiwa juu ya tuhuma za kuachia magari hayo yaliyosheheni sukari ya
magendo.
Taarifa
hizo zimedokeza kuwa askari hao waliokuwa kwenye magari mawili ya FFU, waliitwa
na kuhojiwa ofisini kwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa
Kilimanjaro (RCO), Ramadhan Ng’anzi.
Zaidi
ya magari kumi aina ya Fuso yaliyosheheni sukari ya magendo yamekuwa
yakivuka mpaka kwenda nchini Kenya kila siku kutoka katika mji mdogo wa Himo
kupitia njia ya Kwa Hussein hadi yalipo machimbo ya mchanga aina ya pozolana
mita chache kutoka kituo cha forodha cha Holili na kuingia nchini Kenya
kirahisi.
Mwandishi:
CHARLES NDAGULLA, KILIMANJARO
0 comments:
Post a Comment