Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Muhimbili wamekamilisha awamu ya kwanza ya mpango maalum wa kupeleka huduma kwenye mikoa ya pembezoni ili kusaidia jamii yenye mahitaji sugu yanayohitaji huduma na wataalam, pamoja na Ushauri wa Vipimo.
Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dk. Sonda Shabani, ambapo amesema kuwa jumla ya wagonjwa 250 wamejitokeza kwa lengo la kupata vipimo na matibabu ukiwemo upasuaji.
Mpango huo ambao umeonyesha nia ya kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali kubwa nchini umetoa fursa kwa madaktari kutoa huduma kwa uhakika zaidi kufuatia Mkoa huo wenye Hospitali mbili za Rufaakutokuwa na Daktari Bingwa hata mmoja, hali ambayo imeonyesha ukubwa wa Mahitaji ya huduma za madaktari bingwa katika mikoa mbali mbali hapa nchini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment