Image
Image

DK.SHEIN YUPO KATIKA MJI WA NANJING JIMBO LA JIANGSU CHINA.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiwa wamevalia Vazi Maalum wakati walipoingia katika chumba cha Mitambo ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari, katika Ofisi za Kampuni hiyo Mjini Najing Jimbo la Jiangsu nchini China,katika ziara rasmi ya Kiserikali.[Picha na ramadhan Othman China.]
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kushoto) Mama Mwanamwema  Shein,(wa pili) na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi zake Zanzibar Bibi Chen QiMan, wakimsikiliza Dkt DAI XUELONG, akiwaonesha baadhi ya vifaa vya mawasiliano vilivyotengenezwa na Kampuni ya ZTE,alipotembelea Ofisi za kampuni hiyo akiwa katika ziara ya Kiserikali nchini China katika Mji wa Najing jimbo la Jiangsu.[Picha  na Ramadhan Othman,China.]
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiangalia Mitambo ya Teknolojia ya Mawasiliano ikifanya kazi walipotembelea katika Chumba wakiwa wamevalia Vazi Maalum wakati walipoingia katika chumba cha Mitambo hiyo, katika Ofisi za Kampuni hiyo Mjini Najing Jimbo la Jiangsu nchini China,katika ziara rasmi ya Kiserikali.[Picha na ramadhan Othman China.]
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akifuatana na Makamo wa Rais wa Kampuni  ya Teknolojia ya mawasiliano ya habari (ZTE)  Bibi Chen Jie,wakati alipotembelea  Ofisi za Kampuni hiyo  katika Mji wa Nanjing jimbo la Jiangsu nchini China akiwa katika ziara ya Kiserikali kwa mualiko wa Serikali ya jamhuri ya Watu  wa China.[Picha  na Ramadhan Othman,China
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein katikati wakiwa katika picha ya pamoja na Viongizo wa Kampuni  ya Teknolojia ya mawasiliano ya habari (ZTE) nchini  China,pamoja na ujumbe aliofuatana nao,mara baada ya kuwasili katika Ofisi za kampuni hiyo huko katika Mji wa Nanjing jimbo la Jiangsu nchini China akiwa katika ziara ya Kiserikali kwa mualiko wa jamhuri ya Watu  wa China.[Picha  na Ramadhan Othman,China.]
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein katikati pamoja na ujumbe wake,wakiwa na Mwenyeji Makamo wa Rais wa kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari (ZTE) Bibi Chen Jie,(wa pili kushoto) wakiangalia Simu na kuapata maelezo ya matumuizi ya Simu hizo ,walipotembelea sehemu mbali mbali,akiwa katika ziara ya Kiserikali ya Mualiko wa kukuza ushirikiano katika Nyanja za kiuchumi na Serikali ya jamhuri ya watu wa China,[Picha  na Ramadhan Othman,China.]






Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment