Mkutano huo
utafunguliwa na Waziri wa Sheria na Katiba , Bw. Mathias Chikawe.
Katibu Mtendaji wa
MCT, Kajubi Mukajanga amesema huu utakuwa ni mkutano wa pili kufanyika
hapa nchini, ambapo wahariri wapatao 50 kutoka nchini kote
watahudhuria.
![]() |
| KAJUBI MUKAJANGA - KATIBU MTENDAJI MCT |
Mkutano huo
umeandaliwa mahsusi kuiwezesha MCT na Wahariri ambao ni watendaji muhimu katika
vyombo vya habari, kukutana na kujadiliana kuhusu masuala muhimu
yanayohusiana na taaluma yao pamoja na changamoto ambazo vyombo vya habari
vinakabiliana nazo, na hivyo kuweza kuangalia njia ya kuzipatia ufumbuzi.
Aidha kauli mbiu ya mwaka huu inasema: ìMwelekeo
wa Tasnia ya Habari Tanzania Katika Muktadha wa Kujisimamia Wenyewe.î


0 comments:
Post a Comment