Image
Image

EXCLUSIVE: WIZARA YA MAMBO YA NDANI YATILIANA SAINI NA SERIKALI YA CHINA ILI KUHAKIKISHA INAKABILIANA NA MATUKIO YA UHALIFU WA KIMATAIFA.



Tanzania na China zimesaini  makubaliano ya ushirikiano ambayo yataiwezesha wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Tanzania na wizara ya usalama wa raia ya China kushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo kukabiliana na matukio ya uhalifu wa kimataifa

BAADHI YA WACHINA WAKIWA WAMEKAA HUKU WAKISIKILIZA KWA USTADI , HATUA GANI YA MAKUBALIANO YA UTIAJI SAINI KATI YA TANZANIA NA NCHI YAO.


Kupitia makubalino hayo maeneo yaliyoainishwa ni pamoja na ugaidi, uharamia, biashara ya dawa za kulevya, biashara haramu ya binadamu, usafirishaji wa fedha na wahamiaji haramu.

Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar es salaam ambapo serikali ya Tanzania iliwakilishwa na waziri wa mambo ya ndani Dk. Emmanuel Nchimbi wakati kwa upande wa China aliyesaini makubaliano hayo ni naibu waziri wa wizara ya usalama wa raia bw. Yang Huanning.
YANG HUANNING - NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA USALAMA NA RAIA ( KUSHOTO) DK. EMMANUEL NCHIMBI ( KULIA) WAZIRI WA MAMBO YA NDANI TANZANIA, WAKITILIANA SANAINI.


Kabla ya kusaini makubaliano hayo, mawaziri hao walijadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha ushirikiano katika upande wa mafunzo, ubadil;ishanaji wa taarifa muhimu na upatikanaji wa vitendea kazi.

HUU NI MKONO WA YANG HUANNING - NAIBU WAZIRI WA CHINA AKITIA SANI . 
HUU NI MKONO WA DK. EMANUEL NCHIMBI - WAZIRI WA MAMBO YA NDANI TANZANIA, WAKATI AKITILIANA SAINI YA MAKUBALIANO KATIKA KUBADILISHANA UZOEFU WA KAZI NK.


Licha ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, serikali ya China pia imetoa msaada wa vifaa vya mawasiliano kwa jeshi la polisi ambavyo ni pamoja na radio 150 za mkononi na radio za mezani 160 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 393.

VIFAA VYA MAWASILIANO VILIVYOTOLEWA NA WAKENYA


Kwaupande wake Kamishna mwandamizi wa jeshi la polisi kitengo cha TEHAMA, AMDAN OMAR MAKAME  amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia sana katika kupambana na uhalifu, na akawahakikishia wachina kuwa kwa vifaa walivyotoa watavitumia ipasavyo ili kupunguza vitendo vya uhalifu nchini.

AMDAN OMAR MAKAME - KAMISHNA MWANDAMIZI JESHI LA POLISI .


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment