Image
Image

EXCLUSIVE: WATAALAMU KUTOKA TAASISI YA KIMATAIFA IPO NCHINI TANZANIA KUJADILI UCHIMBAJI MADINI YA URANI.


Timu ya wataalamu watano kutoka taasisi ya kimataifa inayosimamia  nguvu za atomik duniani,IAEA ipo nchini katika majadiliano ya pamoja na wataalamu mbalimbali katika sekta ya nishati na madini wa hapa nchini kuangali kama tumejiandaa vyema kuchimba madini ya Urani.

Washiriki Katika Mkutano huo wakijadiliana kwa Kina ili kufikia lengo.
Akimwakilisha katibu mkuu wizara ya sayansi na teknolojia, mkurugenzi mkuu wa sayansi na teknolojia wa wizara hiyo Profesa, EVELYNE MBEDE ameeleza kuwa ujio wa wataalamu hao wa dunia katika sekta ya uvunaji madini ya URANI,majadiliano yatakayodumu kwa siku 10 utasaidia kama taifa kutambua maeneo gani bado hayajatimiza vigezo katika uchimbaji madini hayo ikiwemo usalama wa binadamu na mazingira.
Prof;EVELYNE MBEDE-mkurugenzi wa sayansi na teknolojia.

Washiriki wakiwa Makini kusikiliza Maadhimio ya Mkutano huo jijini Dar es Salaam.

Prof;IDDI MKILAHA-Mkurugenzi,TAEC.
Akizungumzia maendeleo ya miradi ya utafutaji na uchimbaji madini hayo ya URANI nchini, Mkurugenzi wa tume ya taifa ya nguvu za atomik Prof; IDDI MKILAHA ameeleza pamoja na tafiti kuonyesha maeneo kadhaa ikiwemo maeneo ya BAHI na MANYONI mkoani SINGIDA na DODOMA, lakini mradi uliopiga hatua ni MANTRA wa mto Mkuju,wilayani Namtumbo mkoani RUVUMA ambapo leseni ya uchimbaji na utafutaji imeshatolewa.
Washiriki wa Mkutano huo Wakifuatilia kwa umakini wa Hali ya juu.

ASA MWAIPOPO-mkurugenzi,MANTRA

cue in tc;00;17:16-ASA MWAIPOPO-mkurugenzi,MANTRA.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment