Kambi ya Upinzani Bungeni imeishauri serikali kusitisha uuzaji wa aridhi kwa wawekezaji wa kigeni na kufanya tathimini ili kubaini aridhi iliyokwisha uzwa imeleta tija gani kwa taifa.
Ushauri huo umetolewa bungeni mjini Dodoma na msemaji mkuu wa kambi hiyo kwa wizara ya Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Halima Mdee, wakati wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2013/2014.
Bi. Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, amesema kupitia utafiti uliofanywa katika wilaya 79, unaonyesha kuwa umiliki wa aridhi ni mkubwa kwa wageni kuliko raia, kitu ambacho si kizuri kwa ustawi wa jamii.
![]() |
| Dk. Mary Mwanjelwa - Viti Maalum (CCM) |
Aidha, Mtoa hoja, Waziri wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka alichukua wasaa huo kuzisihi benki za biashara nchini kuanza kuitumia kampuni ya Tanzania Mortgage Refinancing, ili ziweze kutoza riba ndogo kwa ajili ya mikopo ya nyumba.
![]() |
| Profesa Anna Tibaijuka - Waziri wa Ardhi. |




0 comments:
Post a Comment