Image
Image

EXCLUSIVE: CHATU MLA MIFUGO - SONGEA AUAWA


 Na .EMMANUEL MSIGWA,Songea.

Nyoka aina ya chatu anayesadikiwa kuwa mla mifugo katika eneo la Miembeni - Msamala mjini Songea ameuawa baada ya mkazi mmoja wa eneo hilo kupambana naye.

Nyoka huyu mwenye urefu wa futi 12 na nchi 6 ambaye tayari katika windo lake alishamkamata Mbwa na kisha kummeza na kumbakiza sehemu ndogo tu ya miguu ya nyuma  ameuawa majira ya Saa Moja asubuhi kwenye kisima kimojawapo cha Maji ambacho hutumiwa na baadhi ya wakazi wa Miembeni-Msamala mjini Songea kuchota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

CHATU ALIYEKUWA KAMEZA MBWA
MBWA ALIYEKUWA KAMEZWA

Fundi Seremala  aliyejulikana kwa jina la BEDA alisema akiwa nyumbani kwake asubuhi alistushwa na kelele za watoto waliokwenda kuchota maji kwenye Kisima hicho baada ya kumuona nyoka huyo akiendelea na mlo wake wa kummeza mbwa na kwamba alipofika alitaka kukimbia lakini kutokana na panga alilokua nalo mkononi alivaa ujasiri wa kupambana naye na kisha kumuua.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment