TUJIAMINI WAKATI TUKIFANYA, USIOGOPE KWAMBA ETI KUNA ANAYEWEZA ZAIDI KULIKO WEWE LAHASHA, KWANZA JIKUBALI MWENYEWE NDIO WENGINE WATAKUPENDA.
|
Semvua msangi - Akiwa Anafanya kipindi cha Kurunzi la vijana J2,Magic FM |
|
Semvua Msangi - Akiwa anakinukisha Magic FM
Hakika kauli niliyokuwa nimesimuliwa siku za usoni naanza kuiamini kwamba kujituma ndio msingi wa mafanikio sasa naanza kuiona, Hakika safari ni hatua leo hapa kesho pale.
Wakati naanza niliona kama utani vile lakini sasa naanza kuona matokeo yake kwamba Kumbe hata mbuyu ulianza kama mchicha ni kauli yakweli kabisa na yakuaminika, Muungwana mzuri ni yule anaye anza kutambaa kabla ya kutembea.
Maana halisi wapo manyangumi naweza kuwaita hivyo lakini kwa uungwana tu, eti mtu anamkatisha mtu tamaa yakutoweza jambo fulani kuwa hutoweza ila yeye ndiye anaweza kwani kunamtu alizaliwa anajua sote naamini tumefundishwa na waliotutangulia kujua hata vidole havilingani tujue hilo, kiukweli kauli hii huwa inanikera so nakutana na watu mbali mbali wakilalama huku na kule katika sekta fulani fulani jambo la kukatishwa tamaa na watu ambao wanameno katika sekta hizo.
Hivi hebu tafakari kabla yakufika ulipo si ulisaidiwa, ama ulipata msaada waaaina fulani sasa yanini kumkatisha tamaa mwingini, Tubadilike sasa dunia kama mshale wa saa ni haho tu.
|
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment