Image
Image

EXCLUSIVE: KAMBI YA UPINZANI BUNGENI YAISHAURI SERIKALI KUBADILISHA SHERIA ILI MAJANGILI WA TEMBO WANAOKAMATWA WAHUKUMIWE KUNYONGWA


Na . Kuringe Mongi, Dodoma.

Kambi ya upinzani bungeni imeishauri serikali kubadilisha sheria, ili majangili wa tembo wanaokamatwa wahukumiwe kunyongwa, na hivyo kuwaokoa wanyama hao kupotea nchini.

Ushauri huo umetolewa bungeni mjini Dodoma na Kiongozi wa Kambi ya upinzani ambaye pia ni mbunge wa Hai, Bw. Freeman Mbowe, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa mwaka 2013/2014.
Freeman Mbowe - Mbunge wa Hai
Wabunge wengine waliopata fursa ya kuchangia bajeti ya wizara hiyo, ni pamoja na Bw. Felix Mkosamali wa Muhambwe na Bw. Ibrahim Sanya wa Mji Mkongwe, ambao waliitaka serikali kuilinda sekta ya utalii, ambayo inaiingizia taifa fedha nyingi za kigeni.
Felix Mkosamali - Muhambwe
Akijibu hoja za wabunge, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Lazaro Nyalandu amewaahidi wabunge kuwa serikali ina nia thabiti kuhakikisha tembo wanalindwa, na imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na ujangili.
Lazaro Nyalandu - Naibu waziri maliasili na Utalii

Wizara hiyo imeliomba bunge kuidhinishia matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 75.7 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na yale ya maendeleo, kwa mwaka 2013/2014.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment