Mamlaka ya bandari nchini imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa mizigo ya wateja katika bandari ya DAR ES SALAAM, hususan bidhaa za magari ambazo zilikuwa zimefikia hatua ya kukosa mahala pa kuziweka na kusababisha kulundikana eneo moja na kusababisha wizi wa vifaa katika magari hayo.
 |
| Meli Ikiwa Bandarini DSM |
Akiongea na waandishi wa habari eneo la gati namba moja wakati meli moja ya magari ikishusha magari, Kaimu meneja wa bandari, AWADH MASAWE, alisema kuwa hatua hiyo ya kupunguza msongamano wa magari imefanikiwa kutokana na mamlaka hiyo kwa kuongeza muda wa kufanya kazi iliyochangiwa pia na upatikanaji wa vifaa vipya vya kuharakisha kazi.
 |
| AWADH MASSAWE -Kaimu Meneja Bandari |
Amesema kutokana na hali hiyo sasa wana uhakika wa kutoa magari mengi kwa wakati mmoja na hivyo kuokoa muda wa kukaa bandari pamoja na kuzuia wizi na uharibifu wa makusudi ya magari hayo.
 |
| JANETH-RUZANGI-Kaimu Meneja mawasiliano |
cue in.....tc 00:06:20:23(AWADH MASSAWE -Kaimu Meneja Bandari)
Afisa Utekelezaji Mkuu wa Kitengo cha magari yeye alisema kuwa pamoja na kwamba kumekuwepo na ongezeko kubwa la magari yanayoletwa kutoka nje ya nchi,mamlaka imejipanga vyema kuhakikisha inapunguza na hatimae kuondoa kabisa msongamano wa magari bandarini hapo.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment