Image
Image

EXCLUSIVE: HUDUMA YA MIONZI OCEAN ROAD WAGONJWA WASHAURIWA KUZINGATIA RATBA.

Na. Lina Dennis, Dar es Salaam.
Uongozi wa taasisi ya saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es salaam umewashauri wagonjwa wanaofika kwenye taasisi hiyo kupata huduma ya mionzi kuzingatia utaratibu unaotolewa na taasisi ili kuepuka usumbufu wa kusubiri huduma kwa muda mrefu unaotokana na muingiliano wa kutokufuatwa kwa ratiba.
Kifaa kinacho tumia Monzi
X- RAY
Hatua ya uongozi huo imetokana na baadhi ya wagonjwa kufika bila kuzingatia ratiba inayotolewa na hivyo kuwafanya kukaa muda mrefu na hatimaye kulalamikia kinachodaiwa kuwa ni usumbufu unaosababishwa na taasisi.
Ocean Road - Hospital
Muuguzi mlezi wa taasisi hiyo Mary Haule akizungumza katika mahojiano maalum Blogger Hii  amesema uongozi wa taasisi umekuwa na utaratibu maalum wa kutoa ratiba inayoonyesha majina ya wagonjwa, tarehe na muda wanaotakiwa kufika kwa ajili ya huduma ya mionzi lakini baadhi yao hawaufuati na hivyo kusababisha usumbufu.    

Naye mkurugenzi wa taasisi hiyo Prof. Twalib Ngoma akizungumzia huduma katika taasisi hiyo amesema zimeboreka hasa baada ya kuzinduliwa kwa jengo jipya hatua ambayo imepunguza msongamano, ingawa ameeleza kwamba taasisi inakabiliwa na tatizo la mashine za mionzi, kwani zilikuwepo mbili lakini kwa sasa inayofanya kazi ni moja.
Prof. Twalib  Ngoma - Mkurugenzi Mkuu - Taasisi ya Saratani Ocean Road
Kwa sasa taasisi ya saratani ya Ocean Road inauwezo wa kulaza wagonjwa 250 kwa wakati mmoja, hatua iliyopunguza sana msongamano wa wagonjwa ambapo kwa mujibu wa Prof. Ngoma mipango iliyopo ni kuboresha zaidi huduma kupitia utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kudhibiti saratani nchini ambao utatekelezwa kwa awamu kwa kipindi cha miaka kumi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment