Ameyazungumza hayo jana wakati wa
kufungua rasmi mkutano wa kimataifa wa waandishi wa habari mjini Nairobi,
Rais
Kenyatta alisema sekta ya uandishi habari ni kiungo muhimu katika jamii na kwa
mantiki hiyo amevitaka vyombo vya habari kuwajibika zaidi kwa manufaa ya
Wakenya.
Aidha ameonya vyombo vya habari ambavyo hutumiwa na
wanasiasa kuchochea fujo na machafuko kwamba serikali yake haitasita
kuvichukulia hatua kali za kisheria.
Ametoa mfano wa mauaji ya kimbari ya
Rwanda ya mwaka 1994 ambayo yalichochewa zaidi na vyombo vya habari na kusema
serikali haitowavumilia wenye nia ya kuivuruga nchi.
Mkutano huo wa kimataifa
unawashirikisha wanahabari kutoka nchi mbalimbali duniani na unatarajiwa
kumalizika leo hii wakati dunia ikiwa inaadhimisha siku ya kimataifa ya
kutetea uhuru wa wanahabari Duniani kote.
0 comments:
Post a Comment