Jumuiya ya wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu nchini - TAHLISO, imetoa wito kwa wanasiasa nchini kutovigeuza vyuo kuwa maabara za kufanyia majaribio ya falsafa za siasa za vyama vyao badala yake watumie busara kuwahimiza wanafunzi kuheshimu sheria, kanuni na miongozo ya vyuo pamoja na ya nchi.
Akizungumza jijini Dar es salaam mwenyekiti wa TAHLISO, Amon Chakushemeire amesema hatua hiyo ya jumuiya haina nia ya kuwatenga wanafunzi na siasa bali inalenga kuwasaidia kupata muda zaidi wa kujisomea kwani kujihusisha zaidi na siasa kunaweza kukawaathiri kitaaluma.
AMON CHAKUSHEMEIRE.... Mwenyekiti - TAHLISO |
0 comments:
Post a Comment