Kitabu kiitwacho "Njia Ndefu ya Uhuru" kuhusu historia ya rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, kimegusa sana hisia za wasomaji wengi.
Filamu moja iliyotengenezwa kutokana na
kitabu hicho itaoneshwa mwezi Novemba mwaka huu.
Anant Singh, mtayarishaji maarufu wa filamu,
alipata ruhusa ya kutengeneza filami hiyo mwaka 1996.
Picha za filamu hiyo zitapigwa katika miji ya
Johannesburg, Cape Town na kijiji ambacho Mandela alizaliwa.
![]() |
| NELSON MANDELA - RAIS MSTAAFU AFRIKA KUSINI |
Mwigizaji wa Uingereza Idris Elba ataiga kama
Mandela katika filamu hiyo.
Kitabu hicho "Njia Ndefu ya Uhuru"
kiliandikwa kwa siri na Mandela, wakati alipofungwa jela katika kisiwa cha
Robben miaka ya 70 karne iliyopita.
Mwaka 1994, kitabu
hicho kilichapishwa rasmi. Ndani ya kitabu hicho, Mandela alizungumzia historia
yake kuanzia utotoni hadi alipochaguliwa kuwa rais wa kwanza mwafrika wa Afrika
Kusini.
Kitabu hicho
kimetafsiriwa katika lugha mbalimbali na kinapendwa na wasomaji wa nchi
mbalimbali.


0 comments:
Post a Comment