MWALIMU Sophia Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma aliyejifungua watoto watano kwa wakati mmoja kwa njia ya upasuaji mnamo Mei 25 mwaka huu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea na watoto hao kuishi kwa muda wa masaa kumi kabla hawajafariki dunia ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo.
Akizungumza kwa njia
ya simu, Sophia Mgaya akiwa nyumbani
kwake Ruhuwiko mjini Songea alisema alilazimika kuomba kutoka wodini kwa sababu
alikuwa akijisikia uchungu anapowaona wanawake wenzake wodini humo
wakiwakumbatia watoto wao baada ya kujifungua huku wa kwake wote wakiwa
wamefariki dunia baada ya kuzaliwa.
![]() |
|
Hawa
ndio watoto aliojifungua katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma na kesho wakafaliki dunia
(Picha na maktaba)
|
Alisema kuwa muda
wote aliokuwa hospitalini hapo baada ya watoto wake kufariki huku akiwa bado
anauguza kidonda cha upasuaji aliofanyiwa alikuwa akilia muda wote anapowaona
wanawake wenzake waliojifungua wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao hivyo
akaamua kuomba aruhusiwe kutoka hospitalini hapo.
‘’Niliomba
kuruhusiwa kutoka hospitali na kwenda kujiuguza kidonda nyumbani kwa sababu ya
uchungu na majonzi niiiyokuwa nikiyapata wodini hapo ninapowaona wanawake
wenzangu waliojifungua wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao huku wa
kwangu wakiwa wameshazikwa”alisema Bi.Mgaya
![]() |
|
Bi
Jane Mlelwa aliyekaa kitandani akiwa amebeba mmoja wa wawatoto watano
aliowazaa kabla ya watototo hao kufa wote(Picha na maktaba) |
Aidha aliushukuru
uongozi wa hospitali hiyo pamoja na wafanyakazi wote kwa namna walivyomuhudumia
yeye pamoja na watoto wake watano waliozaliwa na kuishi kwa muda wa masaa ya
kumi ambapo alisema kuwa yote yaliyotokea anaamini kuwa ni mapenzi ya Mungu.
Mganga Mkuu mfawidhi
wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma Dkt.Benedict Ngaiza akizungumza na
mwandishi wetu kwa njia ya simu kuwa waliamua kuridhia ombi la mama huyo
kuondoka hospitalini hapo baada ya kujiridhisha kuwa anaendelea vizuri kwa
sababu walifanya kila walichoweza kukoa uhai wake na watoto lakini watoto
walifariki baada ya masaa kumi.
Wakizungumza baadhi
ya wananchi waliomshuhudia mama huyo na watoto wake baada ya kuzaliwa na
kabla hawajafariki walisema kuwa kuna kila sababu kwa kila mwenye uwezo wa
kumsaidia mama huyo kwa namna yoyote afanye hivyo
Bi.Marietha Ngonyani
na Lusi Haule wakazi wa mjini Songea waliwaomba wananchi mbali mbali kujitolea
kumsaidia mama huyo kwa sababu bado anauguza kidonda cha upasuaji aliofanyiwa
na pia tukio hilo limemuathiri kisaikolojia pia hivyo anahitaji faraja.
NA LEWIS MBONDE



0 comments:
Post a Comment