Image
Image

EXCLUSIVE: UMWAGAJI DAMU NCHINI SYRIA HAUKUBALIKI, MJADALA WA DHARURA KUFANYIKA JUMATANO.


Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema jumuiya ya kimataifa inashindwa kutimiza wajibu wake kwa wahanga wa mzozo waSyriakwa kuruhusu vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo kuendelea bila wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria. 

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Uswisi siku ya Jumatatu na kusema kuwa ukiukwaji huo wa haki za binadamu ni sawa na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ambao hauwezi kuachiwa kuendelea bila hatua kuchukuliwa. 
NAVI PILLAY -  KAMISHNA MKUU WA HAKI ZA BINADAMU WA UM
Bi. Pillay amesema vikosi pinzani na serikali vinatumia raia kama ngaoyao katika mapigano ilhali serikali yaSyria inaendelea kutumia nguvu kupita kiasi na kushambulia bila kuchagua hata kwenye makazi ya raia, pamoja na shule na hata hospitali. 

Amesema umwagaji damu na mateso yanyokumba wananchi waSyria yamekuwa hayavumiliki mbele ya binadamu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment