Mkutano wa kwanza wa kikanda wa usimamizi wa amani, usalama
na ushirikiano katika Jamhuri ya kidemokrasia yaCongo, DRC na ukanda wa maziwa
makuu umemalizika hukoAddis Ababa,Ethiopiaambapo taarifa ya pamoja iliyotolewa
mwishoni mwa kikao hicho pamoja na mambo mengine imelaani vurugu zinazoendelea
huko Mashariki mwa DRC.
Taarifa hiyo imesema viongozi wanatambua uwepo wa
vikundi vinavyosababisha vurugu kwenye eneo hilo na kwamba wanaunga mkono hatua
za jumuiya ya kimataifa za kudhibiti vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kupelekwa
kwa brigedi ya kujibu mashambulizi itakayokuwa chini ya ujumbe wa Umoja wa
Mataifa wa kulinda amani huko DRC, MONUSCO.
Viongozi wa nchi hizo kumi ikiwemo
Zambia, Uganda, Tanzania, Sudan Kusini, Afrika Kusini, Rwanda, DRC, Burundi na
Angola wamesema pia wanaunga mkono mpango wa mashauriano baina ya pande husika
ambao utawezesha kufanikiwa kwa mpango wa amani uliotiwa saini huko Addis Ababa
mwezi Februari.
Wamepongeza jitihada za mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa kwenye maziwa makuu, Mary Robinson na vile ambavyo anafanya
mashauriano na serikali ya DRC, serikali za kitaifa, jumuiya za kikanda na za
kimataifa.
Taarifa hiyo imewakariri viongozi hao wakiwasihi wahisani kujitolea
kwa rasilimali ili kuwezesha maendeleo ya ukanda wa maziwa makuu.


0 comments:
Post a Comment