Image
Image

EXCLUSIVE: GAVANA WAKENYA ALILAUMU JESHI LA POLISI LA NCHI HIYO, KWA UZEMBE WA KUSHINDWA KUWALINDA RAIA NCHINI HUMO NA KUSABABISHA KUPOTEZA MAISHA BILA SABABU YA MSINGI.

Gavana wa kaunti ya Garisa  Bw. Nadhif Jama amesema jeshi la polisi nchini kenya ndilo linapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kuwalinda raia wasio kuwa na hatia, ambao wamekuwa wakipoteza maisha kila siku kufuatia mfululizo wa mashambulio ya mabomu ya mara kwa mara katika eneo hilo.

Mapema jana watu watano miongoni mwao  wakiwemo maafisa wawili wa polisi walijeruhiwa baada ya watu waliokuwa na silaha kushambulia vituo vya polisi karibu na mpaka wa Kenya na somalia.

Kiongozi huyo wa garisa alikuwa akizungumza baada ya kukutana na viongozi na wazee wa kaunti hiyo kuzungumzia hali ya amani  ambapo amesema watafanya kila liwezekekanalo kuimarisha hali amani kwa wakazi wa eneo hilo.

Mashambulio hayo yametokea katika miji ya Dadaab na Liboi. Tiyari wakuu wa polisi na viongozi wengine waaandamizi wamekutana kuzungumzia hali hiyo na huku ulinzi makali  ukiimarishwa
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment