Kamanda Diwani akionyesha silaha walizokuwa wakitumia majambazi hao. |
Majambazi wakiwa wamelazwa baada ya kuuawa |
Kamanda Diwani akiangalia gari lililokuwa likitumiwa na Majambazi hao |
Hawa ndio majambazi Waliouawa |
GARI LA MAJAMBAZI HAO |
ASKARI WAKIANGALIA SILAHA
ZILIZOIWEKWA MEZANI ZILIZOKUWA ZIKITUMIWA NA MAJAMBAZI HAO
|
HAO KAMANDA OTHMANI AKISISITIZA JAMBO
BAADA YA KUWATIA NGUVUNI MAJAMBAZI HAYO.
|
MOJA YA SILAHA KUBWA ILIYOKUWA IKITUMIWA
NA MAJAMBAZI HAO IKIWA MEZANI
|
Kamanda diwani akionyesha wskari wenzie moja ya jambazi lililokuwa limeshika silaha |
MTANDAO
wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa baada ya
watu watano wanaodahaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini
kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya Sita Mchana katika kijiji cha
Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.
Alisema
Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na
kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili
T 911 BUG aina ya Toyota Spacio ambapo baada ya kusimamishwa katika eneo
hilo wakitokea Kyela kuelekea Jijini Mbeya.
Alisema
baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo ambapo Askari
walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha
katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari
alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.
Aliongeza
kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki
aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki
nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na
Koa za Shaba.
Kamanda
Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo
yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani
Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.
Aidha
alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana maramoja ambapo
miiliehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi
kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa
taratibu za mazishi.
Pia
anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika
mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.
Picha
na Mbeya yetu
0 comments:
Post a Comment