Akitoa mada juu ya ugonjwa wa malaria wakati wa kongamano la sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS), Profesa Zul Premji, alisema Tanzania inahitaji kati ya dola milioni 300 za Marekani hadi 400, ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo na kusikitika kuwa fedha za kupambana na ugonjwa mara zote zinatolewa na wafadhili badala ya serikali.
Watoto wakiwa ndani ya neti kujikinga na Mlaria |
“Hii
inaiweka vita dhidi ya malaria katika hatari kubwa endapo wafadhili wataamua
kuacha kutoa fedha za msaada au kupunguza kiasi kinachotolewa. “Tanzania ina
uwezo na vyanzo vya fedha vya kufadhili vita hii ya malaria, kama tukiamua
kupanua vyanzo vya mapato ya kodi na kupigana na rushwa kikamilifu,
tutafanikiwa,” alisema Premji.
Hata
hivyo, alisema kuna haja ya kuanzisha mbinu nyingi zaidi za kupigana na malaria
kuliko kutegemea matumizi ya vyandarua yenye dawa ambazo zimeonyesha kushindwa
katika sehemu nyingi nchini ikiwepo Kanda ya Ziwa.
“Inatakiwa
tuangalie ni jinsi gani tutajikinga na mbu si tu vyumbani lakini tukiangalia mbinu
bora zaidi kama tunataka kushinda vita hii dhidi ya malaria.
“Tafiti
zimeonyesha kuwa watu huumwa na mbu jike kabla hawajaenda kulala. Haitaleta
maana kulala ndani ya vyandarua vyenye dawa kabla ya kuyamaliza mazalia ya mbu
kwanza,” alisema.
Wakati
huohuo, Tanzania imeshauriwa kutafuta mbinu za kuwawezesha vijana kiuchumi kama
nchi ina lengo la kushinda vita dhidi ya VVU/ ukimwi.
Akitoa
matokeo ya tafiti katika masuala ya VVU/ukimwi, Profesa Japhet Killeo alisema
kampeni nyingi zimekuwa zikifanyika, lakini vijana wameshindwa kuendana na
mbinu za kujikinga na ugonjwa huo ikiwepo matumizi ya kondomu kutokana na ugumu
wa maisha.
0 comments:
Post a Comment