Image
Image

WATU SABA WAPOTEZA MAISHA BAADA YA BASI LA TAQWA KUGONGANA USO KWA USO NA LORI MUFINDI IRINGA

WATU saba wamefariki dunia papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Kampuni ya Taqwa lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea nchini Zimbabwe, kugongana uso kwa uso na lori la mizigo  katika Kijiji cha Nyololo,Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Taqwa - Picha na Maktaba
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Michael Kamhanda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali hiyo imehusisha basi linalomilikiwa na kampuni ya TAQWA lenye namba za usajili T273CBR linalofanya safari zake kati ya Dar Es Salaam na Zimbabwe na Lori la mizigo lenye namba za usajili T597AMZ.

Kamhanda amesema ajali hiyo iliyotokea ktk kijiji cha Nyololo kilichopo kilomita zipatazo 26 kutoka makao makuu ya wilaya ya Mufindi.
Simu ya Mkononi 
Akilizungumzia tukio hilo mmoja wa manusura wa ajali hiyo ambaye ni rai wa Zimbabwe alisema kuwa  ajali hiyo inasababishwa  na baadhi ya madereva kutokuwa makini wawapo barabarani.

Kwa upande wake  Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Mufindi Erick Bakuza amesema wamepokea maiti saba na majeruhi kadhaa.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment