Mkoani Ruvuma, MAHAKAMA ya Wilaya ya Mbinga imewahukumu watu 23 miaka Saba jela au faini ya shilingi 632,000 kila mmoja kwa tuhuma za kukutwa na nyama ya Nyani iliyoandaliwa tayari kwa kitoweo kinyume cha sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009 kifungu cha Tano.
Kwa wengi si rahisi sana kuamini jambo hili lakini ndiyo hali halisi, Katika mahakama hii ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Mafurushi ya nyama ya Nyani yamefurika na imeelezwa kwamba kwa mizigo hii zaidi ya Nyani 80 wameuawa.
Nyani |
Nikiwa bado katika mahakama hii, watuhumiwa hawa wakaiaminisha jamii kuwa nyama ya nyani inaliwa tena nyama ya paja la mguu wa nyuma ndiyo tamu zaidi kuliko nyama nyingine yeyote.
JUSTINE NDYENABO ndiye Afisa wanyamapori, Pori la Akiba la Liparamba wilayani Mbinga, anasema watuhumiwa hao walikamatwa kijiji cha Luhagara-Mbinga wakisafirisha nyama hiyo kutoka Kihagara Songea ambako ndiko nyani wengi wanapatikana zaidi tofauti na Mbinga ambako kwa sasa wameshapukutika kwa kuliwa.
0 comments:
Post a Comment