Serikali imesema uelewa wa watanzania juu ya umuhimu wa bima ya afya kwa afya zao umeongezeka kufuatia maombi ya taasisi, makampuni na watu binafsi ya kutaka kujiunga na mfuko huo kuongezeka kwa kasi.
Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi ameyasema hayo wakati anazindua bodi mpya ya tatu ya mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF, ambapo amesema pamoja na mwamko wa wananchi kutaka kujiunga na mfuko huo kuwa mkubwa tafiti za taifa za sekta ya afya zinaonyesha kuwa asilimia 40% ya gharama ya sekta ya afya ni fedha zinazotoka kwa wafadhili, asilimia 32% ni fedha kutoka kwenye mifuko ya wananchi, asilimia 26 fedha za serikali na asilimi mbili iliyobaki ndio zinatokana na bima mbalimbali za afya, hivyo bado kunachangamoto kubwa ya kuwafikia watanzania walio wengi.
![]() |
| Dk. Hussein Mwinyi - Waziri wa Afya Tanzania |
Uzinduzi wa bodi hiyo mpya ya NHIF ambayo inawajumbe tisa na itatumikia mfuko huo kwa muda wa miaka mitatu, ilihudhuriwa na wakurugenzi wote wa mfuko huo pamoja na mameneja wa mfuko kutoka mikoa yote ya bara na visiwani.


0 comments:
Post a Comment