Image
Image

EXCLUSIVE: WAZIRI WA ELIMU AENDELEA KUKABWA KOO BUNGENI

Licha ya  serikali kuchukua hatua ya kufuta matokeo  ya kidato cha nne mwaka 2012, lakini bado imesisitizwa kwa waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kujiuzulu wadhfa wake huo na serikali izifidie familia zilizopoteza wanafunzi wao kutokana na matokeo hayo.

Msisitizo huo umetolewa na Mbunge wa Kuteuliwa na Rais Bw. James Mbatia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha (NCCR – MAGEUZI), na kuongeza kuwa maamuzi yaliyofanywa na baraza la mitihani la taifa (NECTA) yalikuwa na msukumo nyuma yake.

James Mbatia - Mbunge wa Kuteuliwa

Shukuru Kawambwa - Waziri wa Elimu Tanzania

Bw. Mbatia ambaye aliibuka bungeni na hoja binafsi ya kutokuwepo kwa mitaala rasmi katika elimu ya Tanzania, na hoja yake kupingwa, amesisitiza kuwa kulikuwa hakuna sababu kwa serikali kuunda tume ya kuchunguza kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne, kwani mambo hayo yalikuwa ni ya kiutendaji na yalikuwa wazi.

Kutokana na serikali kukiri kuwa lipo tatizo katika sekta ya elimu, Mbunge huyo wa kuteuliwa amewataka wabunge wenzake, kubadilika na kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya kuwa na itikadi za vyama, huku taifa likiendelea kuangamia.

Wabunge wa Bunge la Tanzania - Wakiwa Bungeni Dodoma

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment